
Maisha Ni Ramani Inayotokana na Maamuzi Yako;
Kila Siku wewe Huwa na mamia ya Njia na Unapaswa kuchagua mwelekeo kupotia Uchaguzi wako Mwenyewe.
Je, unatumia mda wako?
Unakwenda Wapi?
Unasema/Utasema Nini?…….
Kila Uamuzi Unauwezo wa Kusababisha barabar tofauti na Seti yake ya Maswali. Uwezo wako wa Kuchambua Kati ya Uchaguzi rahisi unaweza Kumaanisha tofauti Kati ya Maisha ya Utajiri na Umasikini, Ugonjwa au Afya, Migogoro au Amani.

Uamuzi Mdogo Unao Ufanya Leo! Unaweza Kuwa Kichocheo kinachokutuma Kwenye Barabara ya Malengo Yako, Ingawa Hautajua Kamwe Umuhimu wa Uchaguzi huu Hadi Kufikia Mwisho wa Safari Yako na Kuangalia Kule Ulikotoka.
Wakati wa Kufanya Maamuzi Sahihi na Muhimu ya Maisha, Vitendo vya Mtu Hutegemea Hukumu yake, Dira Ya Ndani Inayotengenezwa na Ujuzi Wake, Hekima na Uzoefu. Hukumu hufanya Kazi Kama Misuli ambayo inapaswa kutumiwa na Udadisi usio na Mwisho na Tamaa ya Kuelewa Siri za Kina za Ulimwengu huu.
