
Siku Zote Binadamu Hupenda Na Kupendelea Mambo Pekee Waonayo Yanayo Faida Kwa Fikra na Macho Yao, Na Kamwe Hawafanyi Yale Yaliyo na Faida Isiyoonwa Kwa Macho Yao Na Fikra Zao. Atalima Shamba Apande mazao Juu Yake Kwasababu akija Kuvuna Atapata Faida zilizo za Wazi Kwa Mtazamo wa Fikra Zake!!, Mwanafunzi ataenda Shule na Asome Kwa Bidii Akijua Baadaye Atapata Faida Kutokana na Kusoma Kwake….Kutokana Na Kusoma Kwake kwa Bidii.
Mwanadam atakuwa Mwema Kwako Akijua Iko Faida Yoyote Kwako Juu Yake, Atafanya Lolote Liwezekane kwa Sababu tu Jambo Hilo lina Faida Kwake Tu.
Lakini! Wengi wa Wanadam Wamesahau ya Kuwa Wema na Matendo Yaliyo Mame Bila Kujali Hali, Itikadi, Dini, Cheo, Uzima Ndiyo Nguzo Kuu ya Mafanikio na Mema Zaidi Kwetu. Msaidie Ndugu, Rafiki, Jamaa Pasipo Kutegemea Faida Kutoka Kwake Ujaaliwe Upendo, Kheri, Haki na Dhamana Ya Matendo Yako.
Karibu Daima Katika Ardhi Ya Amani.
Freemanbase.
