top of page

Usiogope Mapambano Unayo yapitia Sasa,Yawe Mapambano ya Pesa, Mahusiano, Vita, Njaa…Tambua Daima ya Kuwa Hayo Ni Mambo ya Wakati na Ni Yapitayo pia, Kwa Maana Ni Lazima kwa Kila Mwanadamu Apite Katika Vipindi Upitiavyo Wewe, Hii hutokea Bila kujali Utajiri, Nguvu au Heshima Uliyonayo.
Hakuna Hata Mmoja aliye Juu ya Makwazo,Lakini Daima Tafuta ulinzi wenye Kukufanya utambue ya Kuwa Daima Ni Salama Katika Mwanga(Amani).
Maisha Yako yamejawa na Chaguzi Nyingi Sana zenye kuweza kuamua Juu ya Maisha Yako ya Kesho na Baadaye, Wakati Mwingine Waweza jiuliza Ni Kwanini Mambo Ni Magumu Sana??, Kwanini Wengine tunapambana tu na Wengine wanaishi Vizuri Sanaa? Hii kweli Ni Haki??
Bado haupaswi kuogopa kivuli chako!
Karibu Katika Ardhi Ya Amani.

bottom of page